Rasmi sasa Mbappe ni Mchezaji wa Real Madrid

Staa wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe ni rasmi sasa ataichezea klabu ya Real Madrid msimu ujao baada ya kuthibitika staa huyo atakua mchezaji wa mabingwa hao wa ulaya.

Mbappe amemalizana na klabu ya Real Madrid na ameshaini mkataba na klabu hiyo ambao bado haujawekwa wazi ni wa muda gani, Huku akitarajiwa kutangazwa wiki ijayo kwa maana ya wiki inayoanza kesho Jumatatu.mbappeWinga huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua akitakiwa na klabu ya Real Madrid kwa muda mrefu tangu mwaka 2022 ambapo alikaribia kusaini na klabu hiyo, Lakini hakufanikiwa kujiunga na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Hispania.

Msimu wa mwaka 2024/25 rasmi itakua ni ndoto zilizotimia kwa mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 2018, Kwani ataanza kuitumikia rasmi klabu ya Real Madrid klabu ambayo inaelezwa imekua ndoto ya mchezaji huyo kwa muda mrefu.mbappeKylian Mbappe amejiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure akitokea klabu ya PSG baada ya kumaliza mkataba wake klabuni hapo, Huku taarifa zikieleza mchezaji huyo alishafanya maamuzi ya kujiunga na klabu ya Real Madrid tangu mwezi Febuari mwaka huu.

Acha ujumbe