Polisi Tanzania Yaanza na Makambo

Kikosi cha Polisi Tanzania kimekuwa na msimu mbaya hadi sasa ambapo ndio wanashikilia mkia kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi 9 tuu katika michezo 15 aliyocheza.

 

Polisi Tanzania Yaanza na Makambo

Lakini mabosi wa klabu hiyo waliamua kufanya maamuzi ya kumkabidhi Mwinyi Zahera timu hiyo ya Polisi huku taarifa zikisema kuwa ameanza kumnyatia mshambuliaji wa Yanga.

Zahera aliyewahi kuinoa Yanga, ametua Polisi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Joslin Bipfubusa aliyetemwa hivi karibuni na katika moja ya kazi aliyopewa ni kuleta majembe ya kuinusuru timu hiyo kwenye duru la pili na tayari ameshapendekeza jina moja ambalo ni la Heritier Makambo wa Yanga.

Polisi Tanzania Yaanza na Makambo

Makambo kwa sasa yupo kwao DR Congo alipoenda kwa matatizo ya kifamilia, lakini tayari yupo kwenye rada za Zahera aliyemsajili wakati akiwa Yanga kabla ya kuuzwa AC Horoya ya Guinea na kurejea msimu huu Jangwani, timu ikinolewa na Nasreddine Nabi.

Acha ujumbe