MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa, Mohamed Janabi amezigeukia Yanga, Simba, Azam FC na Coastal Union na kuzishauri kuzingatia zaidi vipimo makini kwa wachezaji wapya watakaowasajili msimu wa 2023/24. Meridianbet ni chimbo la utajiri unaweza kuwa mshindi muda wowote.
Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwezo wa Hospital ya Muhimbili- Mloganzila, katika tukio la kuagana na mchezaji wa zamani wa Yanga, Sunday Manara ambaye alikuwa akifanyiwa matibabu kwenye hospitali hiyo baada ya upasuaji wa goti.
Prof Janabi amezitaka klabu hizo ambazo zinaenda kuwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa, Yanga na Azam FC wakicheza Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba na Coastal Union wakicheza Kombe la Shirikisho ziwekeze zaidi katika suala la kupima afya za wachezaji wanaowasajili, kwa kuangalia maeneo makuu mawili ambayo ni utimamu wa afya ya magoti na moyo.
“Hizi klabu zinatumia fedha nyingi sana kusajili wachezaji hao wa kigeni, kabla ya kuwapa mkataba wanalazimika kuwapima afya zao, Mlonganzila tupo tayari kuangalia afya za wachezaji hao wanaowasajili,” amesema na kuzitaka zisidanganyike na clip za YouTube, bali zizingatie afya.
Itakumbukwa kwamba, Simba na Coastal Union zitaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, huku kwa upande wa Yanga na Azam FC wao watakipiga Klabu bingwa Afrika. Cheza kasino ya Mtandaoni ili uwe moja ya Mamilionea wakubwa Cheza hapa.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.