Ten Hag Kuongezewa Mkataba Mpya

Baada ya taarifa kutoka jana usiku kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ataendelea kuitumikia klabu hiyo kuelekea msimu ujao vyanzo vinaeleza klabu hiyo ina mpango wa kumpa mkataba mpya kocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi.

Erik Ten Hag alikua anahusishwa kwa kiwnago kikubwa kuondoka klabuni hapo na vyombo mbalimbali vya habati nchini Uingereza vilikua vikieleza klabu hiyo imepanga kumtimua kocha huyo, Lakini mambo yamekua tofauti kwani kocha huyo anaendelea kusalia klabuni hapo.ten hagMpaka sasa maongezi ya kumuongezea mkataba mpya kocha huyo yamefika pazuri ambapo pande zote zimekubaliana na kocha huyo ana furaha kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo, Huku wamiliki wao wakipanga kumpa imani kubwa kocha huyo katika mradi wa muda mrefu klabuni hapo.

Kocha huyo ndani ya misimu miwili aliyoitumikia klabu ya Manchester United amefanikiwa kubeba mataji mawili ambapo mataji aliyoyabeba ni Carabao Cup, na FA Cup ambapo ameshinda mwezi uliopita mbele ya mahasimu wao klabu ya Manchester City.ten hagLicha ya msimu mbaya ambao klabu ya Manchester United imekua nao msimu uliopita na kumaliza nafasi ya nane lakini mabasi wa klabu hiyo wameamua kumbakiza Erik Ten Hag, Hii ikiwa na maana klabu hiyo kwasasa haipo tayari kubadili makocha kila wakati na wameamua kumuamini kocha kwa mradi wa muda mrefu klabuni hapo ili aweze kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora wake.

 

Acha ujumbe