Bayern Munich Wapanda Dau kwa Palhinha

Klabu ya Bayern Munich inaelezwa kuongeza dau kwa klabu ya Fulham ili kumpata kiungo wa kimataifa wa Ureno Joao Palhinha ambaye wamekua wakimfukuzia kutoka dirisha kubwa la usajili lililopita.

Bayern Munich wanaelezwa kupandisha dau kutoka dau la awali ambalo walilitoa la kiasi cha €35 milioni ili kuweza kupata huduma ya kiungo huyo wa Kireno ambaye anafanya vizuri sana ndani ya klabu ya Fulham, Lakini pia amekua akionesha kiwango kizuri kwenye timu yake ya taifa ya Ureno.bayern munichMiamba hiyo ya soka ya Ujerumani kwao kinachotakiwa ni kutoa dau ambalo litawaridhisha klabu ya Fulham kwnai mchezaji Joao Palhinha anaonekana kua tayari muda wowote na dili hilo, Kwani mpaka sasa inaelezwa klabu hiyo imeshamalizana na kiungo huyo kwenye suala la maslahi binafsi.

Klabu hiyo ambayo msimu ujao itakua chini ya kocha Vicent Kompany inapanga kuingia sokoni kufanya usajili mzuri ili kuweza kurudisha ubabe wao kunako ligi kuu ya Ujerumani na hata barani ulaya, Ambapo msimu uliomalizika wamepoteza ubingwa wa ligi kuu ya Ujerumani baada ya kubeba takribani miaka 10 mfululizo.bayern munichMsimu ulimalizika ikumbukwe kiungo Joao Palhinha dili lake la kujiunga na klabu ya Bayern Munich liliharibika siku ya mwisho ya usajili, Huku katika hali isiyo ya kawaida alionesha uungwana klabuni hapo na kuamua kusaini mkataba mpaya ndani ya Fulham lakini dirisha hili inaelezwa hataki dili hili licheleweshwe kwakua kiu yake kwa kiwango kikubwa ni kujiunga na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Ujerumani.

Acha ujumbe