Bayern Munich na Palhinha Kila kitu Sawa

Klabu ya Bayern Munich kutoka nchini Ujerumani inaelezwa wamemalizana na kiungo wa kimataifa wa Ureno Joao Palhinha anayekipiga kwenye klabu ya Fulham na wako mbioni kumsajili kiungo huyo.

Kiungo Joao Palhinha yuko tayari kujiunga na wababe hao wa soka la Ujerumani na ameshakubaliana na klabu hiyo suala mshahara na klabu hiyo, Hivo kinasubiriwa ni Bayern Munich kulipa ada ya uhamisho kwa klabu ya Fulham.bayern munichIkumbukwe dirisha kubwa lililopita mabingwa hao wa zamani wa Ujerumani walikaribia kumsajili mchezaji Joao Palhinha lakini dili liliharibika dakika za mwisho kabisa, Jmabo ambalo lilimfanya kiungo huyo kutopendezwa na hali hiyo kabisa na kuilaumu klabu yake ya Fulham.

Kipengele cha mkataba aliosaini Palhinha ndani ya Fulham akitokea Sporting Cp ya ureno kinaeleza klabu yeyote itakayomhitaji inapswa kulipa kiasi cha €45 milioni, Hivo kazi inabaki kwa klabu ya Bayern Munich kulipa kiasi hicho ili kumpata mchezaji huyo ambaye anaonesha ya kuhitaji nia ya kucheza klabu hiyo.bayern munichKama ni Ng’ombe Bayern wamebakiza mkia tu kwani wanatakiwa kulipa kiasi cha pesa tu ambacho kitamruhusu kiungo huyo kuondoka ndani ya Fulham na kuweza kujiunga nao, Klabu hiyo imeonesha kumuhitaji kwa kiwnago kikubwa kiungo huyo kwani licha ya kumkosa dirisha kubwa lililopita lakini wamerudi tena kuhitaji saini yake.

Acha ujumbe