Tuchel Aipiga Chini Man United

Kocha wa zamani wa klabu ya Bayern Munich Thomas Tuchel inaelezwa ameipiga chini ofa ya kuifundisha klabu ya Manchester United kuelekea msimu ujao.

Tuchel inaelezwa alifanya vikao kadhaa na mabosi wa Man United wiki moja iliyomalizika lakini wameonekana kushindwana na kocha huyo, Huku raia huyo wa kimataifa wa Ujerumani akiamua kutofundisha timu yeyote msimu unaofuata.TuchelBaada ya kushindwana na Man United kocha huyo wa zamani wa Chelsea, PSG, na Borussia Dortmund ameamua atachukua likizo na hatafundisha timu yeyote kwa msimu ujao wote, Vyanzo vya ndani kutoka klabu ya Man United vimeeleza kocha huyo alihitaji kiwango kikubwa cha pesa ndio sababu ya kushindwana na mabosi wa klabu hiyo.

Man United ni wazi wamepanga kuachana na kocha Erik Ten Hag kwani mpaka wanafikia kufanya mazungumzo na makocha wengine lengo lao ni kubadilisha kocha, Taarifa zinaeleza pia kumekua na vikao vya ndani vimekua vikiendelea baina ya uongozi na kocha Erik Ten Hag ili kuamua hatma yake.TuchelKocha Robert De Zerbi ni miongoni mwa makocha ambao wako kwenye oridha ya juu kabisa wanaotakiwa na klabu ya Man United, Baada ya Tuchel kuipiga chini Man United mabosi wa klabu hiyo wanaelezwa watahamia kwenye chaguo lingine ambapo ndipo De Zerbi atafata kwani ni moja ya makocha walioko kwenye orodha za juu za mabosi wa klabu hiyo.

Acha ujumbe