Willy Onana na Awesu wamewasili Kambi ya Simba Misri, Lakini bado sura ya Kibu Denis haijaonekana na awali Simba kupitia chanzo kilichopo kambini, kilisema kuwa Kibu Denis Mkandaji alikuwa ameshatua huko.
Lakini ukweli umebainika, walikuwa wanaficha, ila nyota huyo alikuwa hajaenda tofauti na taarifa hizo zilizotolewa wiki iliyopita na kuzua mijadala mtandaoni hadi sasa. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Kwa mujibu wa Mwanaspoti walisema kwamba Kibu aliyemaliza na bao moja na aliyeongezwa mkataba hivi karibuni baada ya kuhusishwa na Yanga, angekuwa mmoja wa wachezaji ambao wangeondoka jana kwenda Misri, lakini hakuwepo katika msafara na kulazimika kudodosa kinachoendelea kwa mchezaji huyo.
Hata hivyo, imeelezwa Kibu bado hajarejea nchini akiendelea kula bata Miami Beach, iliyopo Jiji la Florida na haijawekwa wazi kitu gani kinachomfanya ashindwe kuungana na wenzake kambini kwani wachezaji wote wakiwamo wapya na wa zamani wameshaungana pamoja ukimuondoa Aishi Manula.
Katika kudodosa taarifa za Kibu Denis, mtu wa karibu na mchezaji huyo alisema, ana ruksa maalumu, kwani alimaliza Ligi Kuu msimu uliopita akiwa majeruhi, hivyo anaendelea kujiuguza kabla ya kuja kuungana na wenzake.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi zinakaribia kuanza, usije kupishana na gari la Mshahara.
“Ni kweli hajaenda kambini, ila ana ruksa maalumu kwa vile aliumia kabla ya msimu kumalizika na anajiuguza na viongozi wamekuwa wakiwasiliana naye, lakini bado hajapona, hivyo hata akienda huko hatakuwa na la kufanya, lakini utafute uongozi utakupa majibu zaidi,” kilisema chanzo hicho.
Kibu mwenyewe alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi huo wa kukosekana kwake kambini, hakuwa tayari kusema lolote akitaka watafutwe viongozi. “Sina la kusema, we watafute viongozi,” alijibu Kibu kwa kifupi na Mwanaspoti lilipomsaka Mratibu wa Simba, Abbas Ally alisema yeye sio msemaji.
Kwa upande wa Afisa Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally alitafutwa kuelezea taarifa hizo lakini hakuweza kufanikiwa kwa sababu hakupokea wala kujibu meseji alizotumiwa.
Lakini Pia kiongozi huyo alidokeza kampeni za uzinduzi wa tamasha la Simba Day na Jezi mpya kwa msimu wa 2024/2025 sahau kwani Mnyama anafanya mambo yake kimya kimya ili wawasapraizi wengi.
Jezi hizo zinatarajiwa kuwa na mabadiliko kadhaa ya chapa za wadhamini na wiki ijayo itakuwa ya moto kwa Simba kwani itazindua rasmi kampeni za tamasha la Simba Day ambalo kilele chake kitafanyika Agosti 03, Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.