Klabu ya Manchester United sasa inatarajiwa kurudi kwa mlinzi wa klabu ya Everton raia wa kimataifa wa Uingereza Jarrad Branthwaite ambaye dili lake lilishindikana siku kadhaa nyuma.
Baada ya kumsajili beki Leny Yoro kutokana Ufaransa Manchester United inaelezwa bado inahitaji kufanya usajili wa beki mwingine wa kati ndani ya klabu hiyo, United wanatarajiwa kurudi kwa Branthwaite kutokana na hali ya kiuchumi ambayo klabu ya Everton inapitia wakati huu.Everton ilikua ina mpango wa kuuzwa wiki kadhaa nyuma ambapo mazunguzmo yalikua yakiendelea baina ya wamiliki wa sasa wa klabu hiyo dhidi ya matajiri wapya ambao walitaka kununua hisa kubwa klabuni hapo wanaofahamika kama Friedkin Group ambapo mchakato huo umefeli, Kupitia hali hii Man United wanamini ndio nafasi ya kurejea na na kumsajili Branthwaite kutokana na hali ya kiuchumi ya Everton.
Klabu ya Everton ilipiga chini ofa za klabu ya Man United mara mbili kutokana na kile kilichoelezwa kua hawakufiki kiwango halisi ambacho Everton walikihitaji, Lakini kupitia kufeli kwa mchakato wa ununuzi wa klabu hiyo ni wazi watakua hawako kwenye hali nzuri kiuchumi na ndio nafasi ambayo United wanaitegemea zaidi.
Beki Jarrad Branthwaite inaelezwa alishakubaliana maslahi binafsi na klabu ya Manchester United lakini tatizo lilikua klabu ya Everton ambayo iliweka ugumu ambapo walihitaji dau kubwa kwa beki huyo, Lakini Man United wanaelezwa wanatarajia kurejea kwenye mawindo ya beki huyo wakiaminini Everton wanaweza kukubali dau walilotuma mwanzo kutokana na hali yao ya kiuchumi.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.