Chelsea Wanamvizia Lunin

Klabu ya Chelsea inaelezwa ina mpango wa kumsajili golikipa namba mbili wa klabu ya Real Madrid Andrey Lunin kwajili ya kua golikipa namba moja ndani ya klabu hiyo msimu ujao.

Chelsea inaelezwa haina mpango wa kumbakiza Kepa ndani ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao licha mkataba wake wa mkopo kumalizika ndani ya klabu hiyo, Huku wakimuona Lunin kama mtu sahihi ambaye atakuja kuongeza kitu kipya kwenye eneo lao la golikipa.chelseaGolikipa huyo wa Ukraine amekua kwenye kiwango bora sana msimu uliomalizika ndani ya klabu ya Real Madrid akirithi vyema mikoba ya Thibaut Courtois, Hivo Matajiri hao wa London wanaona kipa huyo ana uwezo kufanya makubwa klabuni kwao na ndio sababu ya kumuhitaji.

Klabu ya Chelsea inaweza kutumia faida ya Lunin kuhitaji kucheza ndani ya Real Madrid kumpata kwani golikipa Lunin inaelezwa anaipa nafasi Real Madrid, Lakini sharti ni muda zaidi wa kucheza jambo ambalo linaonekana kua gumu kwakua bado Real Madrid wanaamini Courtois ataendelea kua namba moja klabuni hapo.

Acha ujumbe