UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa hesabu kubwa kwasasa ni kupata pointi tatu mbele ya Coastal Union wakiwa ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kupoteza mchezo uliopita Uwanja wa Jamhuri, Morogoro dhidi ya Tanzania Prisons.
Ipo wazi kwamba mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza ilikuwa dhidi ya Yanga, Novemba 5 2023 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga kete ya pili kupoteza ilikuwa ni Machi 6 2024, Simba 1-2 Tanzania Prisons.Mechi zote Simba ilipoteza ikiwa nyumbani ndani ya msimu wa 2023/24 baada ya kucheza mechi 16 imefikisha pointi 36ikiachwa kwa tofauti ya ointi 10 na Yanga yenye pointi 46 kibindoni.
Simba wanatarajiwa kucheza na Coastal Union ya Tanga leo Jumamosi,Uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni mzunguko wa pili na ipo wazi kwamba Coastal Union wametoka kugawana pointi mojamoja na Azam FC walipofungana bao 1-1, Uwanja wa Azam Complex.
Ahmed Ally, Meneja Idara Habari wa Simba amesema wanakwenda kupambana na Coastal Union wakiwa na machungu ya kupoteza pointi tatu mchezo uliopita.
“Tunatambua ushindani ni no mkubwa tunawakabili wapinzani wetu Coastal Union tukiwa na machungu ya kupoteza mchezo wetu uliopita.”