BAADA ya kujifua kwa muda wa wiki mbili sasa katika kambi iliyopo Ismailia, Misri kikosi cha Simba chini ya kocha mpya, Fadlu Davids leo jioni kitashuka uwanjani kutesti mitambo dhidi ya El Qanah ya nchini humo. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Mechi hiyo ya kwanza ya kimataifa ya kujipima ngumu itapigwa kuanzia saa 11:30 jioni kwenye uwanjani uliopo kwenye kambi hiyo, ikiwa sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano na nafasi ya kocha Fadlu kuwasoma vyema mastaa wa timu hiyo na kurekebisha makosa mapema kabla ya kurudi nchini.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi zinakaribia kuanza, usije kupishana na gari la Mshahara.
Kocha huyo alinukuliwa na mtandao wa klabu ya Simba, akijivunia kikosi alichoancho kwa jinsi kilivyo na ushindani unaompa picha ya kufanya vizuri msimu ujao, ingawa itakuwa mara ya kwanza kwake kufanya kazi Ligi Kuu Bara.
Fadlu alisema ameuona uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na alishaanza kuwapa mazoezi ya kimbinu, ufundi ili kupata timu itakayokuwa na uwezo wa kufanya vizuri wakati wa mashindano mbalimbali.
Kocha huyo aliyasema hayo, wakati anafanya mahojiano na mitandao ya kijamii ya Simba, alisema “Ushindani ni mkubwa, kila mchezaji anajituma, nimefanikiwa kuona uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, hilo ni jambo muhimu, kwani nakuwa najua jinsi ya kuwatumia. Ninachokifanya kwa sasa ni mazoezi ya mbinu na ufundi, ili kupata timu itakayokuwa na uwezo mkubwa wa kupata matokeo katika mashindano mbalimbali.”
Kocha huyo alisema ni kazi yake kuona kila mchezaji anafanya vizuri na kufurahia kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.
“Ni kazi yangu kila mchezaji kushaini katika nafasi yake, ndio maana kila mmoja namuelekeza katika nafasi yake jinsi ya kutekeleza majukumu yake, pia nitaendelea kuwaona katika mechi mbalimbali ambazo tutacheza hapa zinaweza zikawa tatu,” alisema kocha msaidizi huyo wa zamani wa Raja Casablanca ya Morocco.
Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.