SINGIDA FOUNTAIN GATE IMENOGA KWELIKWELI

SINGINDA Fountain Gate imewatambulisha majembe mapya yatakaokuwa ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa msimu wa 2023/24.

Miongoni mwa nyota wapya ni wale waliokuwa ndani ya Simba na Yanga kwa msimu wa 2022/23.

Ukiweka kando Joash Onyango ambaye alikuwa ndai ya Simba pia wamemtambulisha mshambuliaji Habib Kyombo na amepewa jezi namba 10.

Mwamba mwingine ni Thomas Ulimwengu hii ni zawadi kwa Singida Fountain Gate kwa kuwa hakuwa kwenye tetesi za awali.
Beno Kakolanya ni kipa uhakika kuwa kwenye anga la kimataifa msimu wa 2023/24 akipata changamoto mpya ndani ya Singida Fountain Gate.

Ikumbukwe kwamba Kakolanya alikuwa anacheza ndani ya Simba atakuwa kwenye changamoto mpya msimu wa 2023/24 kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Dickson Ambundo aliyekuwa ndani ya Yanga alikuwa anatajwa kuibukia Dodoma Jiji ni mali ya Singida Fountain Gate na Kelvin Kijili kutoka KMC ni mali ya Singida Fountain Gate

Acha ujumbe