Kuhusu Ujenzi wa Uwanja, Injinia Hersi Afunguka Kila Kitu

RAIS wa Yanga SC, Injinia Hersi Said amesema kuhusu mipango ya kujenga uwanja wao wa kisasa katika eneo la Jangwani, walipewa machaguo mawili, walipwe fidia na kuhama katika eneo hilo ambalo liko katika mipango ya kuboreshwa au wajenge uwanja ulio bora kabisa. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Injinia Hersi aliyasema hayo jana alipokuwa akihutbia wanachama na mashabiki wa timu hiyo, katika mkutano mkuu wa mwaka, ambapo ulihusiana na ukaguzi wa hesabu za matumizi kwa msimu mzima, na kupitisha bajeti kuu ya klabu hiyo mwaka 2024/25 ambayo inafikia Bilioni 24 za kitanzania. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

“Serikali ilitufanya tuchague mambo mawili, kuachia uwanja ili turudishiwe fidia ama kujenga uwanja wa kisasa utakaoendana na eneo hilo, tulichagua namba mbili na sasa naamini Yanga itakuwa na uwanja wa kisasa hapa nchini.”

“Tunamshukuru mzee wetu aliyetangulia mbele ya haki, Abeid Amani Karume aliyejenga jengo hilo mwaka 1971, lakini kila kitu kinatakiwa kufanyiwa marekebisho na sasa Yanga ndio iliyo na jengo la kisasa kuliko klabu zote Tanzania na kama siyo Afrika.

Mbali na hilo, alizungumzia msimu ujao (2024/25), kwamba watakuwa na msimu bora kuliko uliopita.

“Msimu bora unaanzia na usajili, tutakuwa na benchi bora kuliko la msimu uliopita, tutakuwa na wachezaji bora, kila mwaka tutaongeza wachezaji wenye ari na mafanikio, hatuwezi kubweteka kutokana na mafanikio tuliyopata, tutakuwa na kambi nzuri, tumealikwa Iran, Afrika Kusini na Kenya kufungua uwanja wao mpya wa kisasa,” alisema Injinia Hersi.

Timu hizo ni Kaizer Chief FC na Gor Mahia ya Kenya.

Kwa kauli ya rais wa Yanga ni kama inakoleza moto wa kocha wao Muargentina, Miguel Gamondi ambaye bado hajasaini mkataba mpya na tetesi nyingi zinamzunguka ikiwamo kutakiwa na klabu nyingine.

Acha ujumbe