Tajiri MO Dewji, Aapa Kufia Simba! Kina Nani Wanataka Kumuondoa?

Mohammed Dewji (Mo Dewji) ambaye ni Rais wa Hashima na Muwekezaji wa klabu ya Simba amesema kwamba hawezi kuiacha timu hata iweje. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

MO Dewji ameibuka kwa kasi sana mitandaoni, na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kufikiria mambo mengi juu ya kinachoendelea ndani ya klabu yao. Huku wengine wakihofia huenda tajiri huyo akaiacha timu yao.

Simba imekuwa katika sintofahamu kwa kipindi cha siku tatu mfululizo, huku wajumbe wa bodi upande wa wanachama wakifichua namna wanavyopata wakati mgumu wa kuafiki mawazo ya Mo katika uwekezaji wa klabuni hapo.

Wikiendi hii imekuwa na heka heka mitandaoni na kwa mashabiki wa Simba baada ya Mo Dewji kuandka katika ukurasa wake instagram ujumbe unaosomeka: Kujikwa si kuanguka, bali ni kwenda mbele. Simba Tupo Pamoja!

Lakini pia kupitia insta stori yake MO Dewji aliposti wimbo wa msanii Tunda Man “Tambeni” ukituma ujumbe wa kwamba “Mtanipiga mpaka mniue mimi Simba Sihami”

Bila shaka MO Dewji anajaribu kuwaambia mashabiki kile kinachoendelea ndani ya klabu hiyo kwa sasa, kitu ambacho kinaifanya timu hiyo kushindwa kupiga hatua zaidi.

Taarifa tulizozinyaka zinaeleza kwamba, kuna nguvu inatumika kubwa tu ya kumkwamisha muwekezaji ili aondoke klabuni hapo, na timu apewe kigogo mmoja kutoka upande wa pili. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

Acha ujumbe