Jean Baleke Anasubiri Simu Kutoka Simba & Yanga

SIMBA na Yanga, zinaweza zikaingia vitani kuwania saini ya straika Jean Baleke wa Al-Ittihad ya Libya, baada ya kuwepo na taarifa kufuatwa na viongozi wa klabu hizo. Bashiri na Meridianbet hapa.

Baleke alijiunga na Al-Ittihad, akitokea Simba ambapo kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam na tetesi za kuhitajika na hizo klabu zimekuwa kubwa.

Siku ya Jana alikuwa kwenye uwanja wa Azam Complex kucheki mchezo wa Simba Queens, ambapo alionekana kwenye picha ya pamoja na Mjumbe wa Simba Asha Baraka.

Baleke alizungumiza hatma yake ya kureejeea Tanzania huku akibainisha kuwa yupo tayari kujiunga na timu yeyote hapa Tanzania. Beti na Meridianbet kwa uhakika wa ushindi na maokoto, Odds kubwa na machaguo 1000+

“Tanzania ni nymbani ila bado nina uraia wa Congo DR, Nimerudi hapa kuchukua vitu vyangu, Nasikia watu wanazungumzia kuhusu mimi kucheza Yanga, wengine wanasema njoo Yanga, Njoo Azam, Rudi Simba,timu yeyote ikinipigia niende nanda. Hata Simba wakinipigia simu nirudi nipo tayari kurudi” Jean Baleke

Aidha mchezaji huyo ambaye aliondoka Simba akiwa na mabao 8, amezungumzia juu ya mkataba wake na klabu yake ya sasa Al-Ittihad ya Libya kwamba ulikuwa wa mkopo wa mwaka mmoja, katumikia miezi sita, imebakia sita, hivyo lolote linaweza likatokea.

Baleke ndiye mfungaji bora wa ligi ya Libya, alimaliza na mabao 14, alicheza mechi nane na alifunga hat-trick nne.

Acha ujumbe