VIBALI AZAM, YANGA,SIMBA IPO HIVII

BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuweka wazi kuwa wachezaji wa kigeni wa timu mbili za Singida Fountain Gate na Simba hazijawasilisha vibali vya wachezaji wa kigeni Simba imetoa taarifa nyingine.

Agosti 10 mapema TFF ilitoa taarifa kuwa Klabu za Singida Fountain Gate na Simba ndio klabu pekee ambazo hazijawasilisha kibali cha mchezaji yoyote wa kigeni.SIMBAMiongoni mwa wachezaji wa kigeni waliopo ndani ya timu hizo ni Bruno Gomes, Meddie Kagere hawa wapo ndani ya Singida Fountain Gate huku Fabrice Ngoma, Luis Miquissone hawa NI baadhi ya waliopo ndani ya Simba.

Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa tayari wamekamikisha vibali vyote na wachezaji watakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate.

Simba na Singida Fountain Gate watamenyana katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii ya pili Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Ni Yanga wametangulia fainali baada ya ubao wa Uwanja wa Mkwakwani kusoma Yanga 2-0 Azam FC.SIMBATaarifa kutoka TFF imeeleza kuwa Yanga imekamilisha tayari vibali sawa na Azam FC ambazo hizi zilianza kutupa kete Agosti 9.

Yanga inamsubiri mshindi wa mchezo wa leo ili kujua mpinzani wake watakayecheza fainali Agosti 13.

Acha ujumbe