Klabu ya Yanga ambao ndio vinara wa Ligi kuu ya NBC wanatarajia kushuka dimbani kesho kukiwasha dhidi ya Ihefu ambao mechi ya kwanza walifungwa bila kuamini macho yao.

Yanga watawakosa baadhi ya wachezaji wao muhimu hapo kesho akiwemo Aziz KI, Bernad Morisson, na Yanick Bangala kwa sababu mbalimbali ambazo hazijaorodheshwa na kocha msaidizi Cedric Kaze.
Young Africans wapo juu kileleni kwenye msimamo wa Ligi wakiwa wamecheza mechi zao 19, wakishinda mechi zao 16, sare 2 na kupoteza mechi moja pekee ambayo ni dhidi ya Ihefu.

Nahodha wa timu hiyo Bakari Mwamnyeto amesema kuwa wamejiandaa kukusanya pointi zote tatu hapo kesho na watacheza kama wanavyokuwa wanacheza na timu zingine, huku mchezo huo ukipigwa Benjamin Mkapa majira ya 12:30 jioni.

