Yanga Yaeleza Malengo Yao ya Usajili

Uongozi wa Yanga umesitiza juu ya kumalizana na wachezaji wote ambao walikuwa wakiwahitaji, huku wakiweka wazi kuwa hakuna mchezaji mwingine yeyote ambaye walikuwa wanamhitaji ambaye hawajamalizana naye.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya NBC mpaka sasa wamemtambulisha mchezaji mmoja, mzawa winga Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate alikokuwa kwa mkopo akitokea Mtibwa Sugar huku kwa wachezaji wa kigeni wakiwa bado hawajaanza kazi.

YangaYanga wanahusishwa kukamilisha usajili wa wachezaji wengine kama Maxi Mpiana kutoka DR Congo, Jonas Mkude aliyeachwa Simba SC na Mohamed Zougrama na Yao Kouassi kutoka Asec Mimosas huku pia wakihisishwa na Mshambuliaji kutoka Ligi kuu ya Ghana,

Makamu wa Rais wa mabingwa hao watetezi wa ligi ya NBC, Arafat Haji amesema kuwa wao kama uongozi tayari walishakamilisha usajili wa wachezaji wote ambao walikuwa wakiwahitaji hivyo hakuna mchezaji mwingine ambaye wanamfukuzia kwa sasa.

“Wananchi tayari tumekwishamaliza taratibu zote za kuwasajili wale wachezaji wote ambao tulitaka kuwasajili kwa msimu huu hivyo hakuna mchezaji mwingine yeyote ambaye tunamhitaji na tunamfuatilia.Yanga“Kwa sasa ambacho tunakifanya ni kuhakikisha kuwa tunafuata taratibu zetu za utambulisho kupitia kitengo chetu cha habari na mawasiliano, kwani ndio jambo ambalo linafuata muongozo wa kiofisi na makubaliano ya ukuaji katika sekta hiyo ya habari ya Yanga,” amesema kiongozi huyo.

Acha ujumbe