Fainali ya AFCON 2021 inapigwa leo katika dimba la Olembe unaopatikana kwenye mji kuu wa Cameroon, Yaounde. Nyota wawili wa Anfield ya England watakutana kuoneshana ubabe katika mchezo unaotarajiwa kushuhudiwa na wapenda soka wengi ulimwenguni.
Senegal imetinga fainali ya pili mfululizo ya AFCON wakisaka taji la Afrika na safari hii watavaana na Misri ambayo iliwaondoa wenyeji Cameroon kwa mikwaju ya penalti 3-1 katika hatua ya nusu fainali.
Fainali hii itakuwa ni ya nyota wawili wa kutoka Liverpool ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa tishio haswa kwa magolikipa wengi barani Ulaya. Sadio Mane na Mohamed Salah ndio roho za timu zao wakiwa na mchango mkubwa mpaka kuzifikisha timu zao fainali za AFCON.
Mane amecheza jumla ya dakika 520 kwenye michuano hii amechangia mabao matano, akifunga matatu na kutoa asisti mbili ikiwemo ya nusu fainali dhidi ya Burkina Faso na kuipa Senegal ushindi wa mabao 3-1.
Mo Salah amecheza mechi zote kwa dakika zote 630 kwenye mashindano haya, yeye amechangia mabao matatu akifunga mawili na kutoa pasi iliyozaa bao kwenye mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Morocco.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.