Kikosi cha Simba SC kitashuka leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao utaanza saa moja usiku.
Katika mchezo wa leo Simba SC anahitaji alama tatu muhimu ili kuendelea kupunguza tofauti ya alama kati yetu na watani wao wa jadi Yanga SC ambao walitoka suluhu ya 0-0 jana.
Kocha Msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amesema tunatarajia kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Mbeya Kwanza na tutaipa heshima kubwa ili kutimiza lengo letu la kupata alama.
“Mechi haiwezi kuwa rahisi na tunalijua hilo. Mbeya Kwanza ni timu nzuri tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kubaki na alama zote tatu.
“Tunajua suala la ukame wa mabao lipo kikosini, benchi la ufundi tumelifanyia kazi mazoezini na tunategemea kuanzia mchezo wa leo mabadiliko yataanza kuonekana,” amesema Matola.
Kiungo mkabaji wa Simba SC, Sadio Kanoute ambaye alikosa mechi mbili zilizopita amerejea kikosini na amefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa leo.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.