Klabu ya Al-Nassr ni kama wamehamia klabu ya Manchester United na kujichukulia wachezaji ambapo mpaka sasa wameshachukua wachezaji wawili na sasa wanamuhitaji Eric Baily.
Beki Eric Baily mchezaji wa Manchester United ambaye alikua kwa mkopo msimu mzima klabu ya Olympique Marseille anatakiwa na Al-Nassr ambao wanatajwa kuweka kiasi cha paundi milioni 20 ili kumpata beki huyo.Baily ameshindwa kupata nafai ndani ya klabu ya Manchester United kutokana na majeraha ambayo yalikua yanamkabili mara kwa mara, Ambapo mashetani wekundu hao wakaamua kumtoa kwa mkopo kwa Marseille ya nchini Ufaransa.
Mkopo wa Eric Baily umemalizika na Olympique Marseille ambapo beki huyo hayupo kwenye mipango ya kocha Ten Hag na amewekwa sokoni, Huku Al-Nassr wao wakionesha kuvutiwa na beki huyo na kuhitaji saini yake.Alex Telles amejiunga na klabu ya Al-Nassr akiungana na Cristiano Ronaldo ambaye alijiunga mwezi Januari na sasa wamehamia kwa beki Eric Baily ambaye wameweka dau la paundi milioni 20 ambalo inaelezwa kua Man United hawawezi kukataa ofa hiyo.