Klabu ya Aston Villa chini ya kocha Unai Emery ipo makini kwelikweli kwenye dirisha hili la usajili kwani mpaka sasa imefanikiwa kusajili wachezaji watatu muhimu.

Aston Villa inafahamika wanaboresha timu hiyo kuelekea msimu muhimu kwao kwasababu watakua kwenye michuano ya ulaya msimu ujao hivo ndio sababu inayofanya wahakikishe wanakiboresha kikosi chao kwa kiwango kikubwa.Aston villaUnai Emery tangu ametua kwenye kikosi hicho ameibadilisha klabu hiyo kwa kiwango kikubwa sana, kwani klabu hiyo ilikua kwenye kipindi kigumu chini ya Steven Gerrard lakini baada ya Emery ikakaa sawa mpaka kufuzu michuano ya ulaya.

Aston Villa wamemuongeza mchezaji Youri Tielemans kwa uhamisho huru kutoka Leicester City beki Pau Torres kutoka Villarreal kwa ada ya puandi milioni 35, pamoja na kiungo Moussa Diaby kutoka Bayern Liverkusen ambapo dau halijawekwa wazi.Aston villaUsajili ambao wameufanya Aston Villa moja kwa moja unaonekana una lengo la kwenda kutibu maeneo toauti tofauti kiwanjani huku ikiwa ni moja ya vilabu vilivyofanya usajili wenye mantiki kuelekea msimu ujao wa ligi kuu ya Uingereza na michuano mingine.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa