Ancelotti: Kroos na Modric Hawachezi kwasababu ya Majina bali ni Uwezo

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kua viungo wake wawili wakongwe Luca Modric na Toni Kroos hawachezi ndani ya klabu hiyo kwasababu ya majina yao lakini inatokana na uwezo wao.

Kocha Ancelotti aliyazungumza hayo jana baada ya mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Liverpool katika usiku wa ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo Real Madrid walifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Liverpool kwa jumla ya mabao 6-2.ancelottiLuca Modric na Toni Kroos wamekua kwenye kiwango bora kwa muda mrefu ndani ya klabu ya Real Madrid, Huku wengi wakifikiri uwezo wao labda umemalizika lakini Ancelotti haaamini hivo yeye anaona wachezaji hao wanacheza kutokana na ubora ambao wanaendelea kuuonesha kila siku.

Toni Kroos na Luca Modric walicheza jana dhidi ya klabu ya Liverpool na wakionesha kiwango cha hali ya juu wakiwa sehemu ya silaha muhimu iliyotumika kuiangamiza klabu ya Liverpool, Kutokana na ubora ambao wanauendeleza ndani ya klabu hiyo imepanga kuwapa mkataba mpya.ancelottiKlabu ya Real Madrid ipo kwenye mazungumzo na viungo hao wawili kuhakikisha wanasalia ndani ya klabu hiyo, Viungo hao wanatarajia kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja ili kuendelea kuwatumikia wababe hao wa soka barani ulaya.

Acha ujumbe