Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta amefurahishwa na kiwango cha kapteni wa klabu hiyo Alexander Lacazette katika mechi za hivi karibuni ambazo amekuwa akianza katika kikosi cha kwanza.

 

Arteta, Arteta Afurahishwa na Kiwango cha Lacazette., Meridianbet

 

Arteta amefurahishwa zaidi baada ya jana mshambuliaji huyo kutengeneza nafasi mbili (assist) za magoli katika ushindi wa 3-2 ugenini dhidi ya Watford wanaopambana kutoka mkiani.

Mkataba wa sasa wa Lacazette unaisha mwishoni mwa msimu na kumekuwa hakuna mazungumzo yoyote ya kuongeza mkataba mpya mpaka sasa.

Kiwango cha mfaransa huyo kimeibua mapendekezo ya kuongezewa mkataba wa kuendelea kucheza katika kikosi hicho msimu ujao lakini Arteta amesema hatma yake itajadiliwa baadae msimu huu.

“Nadhani amekuwa na wakati mzuri sana katika masuala ya rekodi za ufungaji mabao, pengine bora kuliko anachofanya hivi sasa, lakini kwa kile tunachomuomba na kwa kile ninachomuomba na mchango ninaohitaji kutoka kwake, nadhani anaendelea vizuri, vizuri sana.” Arteta aliwaambia waandishi wa habari.

 

“Ndivyo ilivyo. Niliwaambia, mwisho wa msimu tutakapojua tulipo, tutakaa na wale wachezaji watatu [walio nje ya mkataba] na kati yetu sote, tutaamua nini cha kufanya ili kusonga mbele. .” aliongeza.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa