Wakati jahazi la Manchester United likiwa halieleweki ni wapi linaelekea, Marcus Rashford anaungana na baadhi ya wachezaji wa United wanaojifikiria mara mbili kule OT.

Old Trafford kunaendelea kuwa pachungu kwa mashabiki, uongozi na wachezaji wa Manchester United. Msimu huu ndio umekua kama shubiri kwao, hii ni kutokana na matokeo mabovu uwanjani.

Awali, Ole Gunnar Solskjaer na benchi lake walionekana ndio kikwazo kwa United, wameondolewa (amebaki Mike Phelan pekee) na mambo ni yaleyale. Matokeo ya United chini ya Ralf Rangnick bado hayatoi tumaini la mafanikio msimu huu.

Rashford (wengine wakampa jina la “Mtoto wa Ole”) amekua na wakati mgumu zaidi msimu huu. Awali alikua na majereha ya bega, alifanyiwa upasuaji na kukaa nje ya dimba kwa muda. Baada ya kurejea kwake, imekua tofauti na ilivyotarajiwa. Bora kile kiwango wakati anamajeruhi kuliko kiwango cha sasa.

Rashford, Rashford Anajifikiria Mara Mbili Kule OT, Meridianbet

Paul Pogba, Juan Mata, Edinson Cavani, Jesse Lingard, Anthony Martial, Dean Henderson na Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji ambao wanazitafakari nafasi zao ndani ya kikosi cha United. Huenda huu ukawa ni msimu wa mwisho kuwaona wachezaji hawa kwenye usi wa rangi nyekundu kule Old Trafford.

Licha ya kuwa na mkataba na United mpaka 2023 (unaoweza kuongezwa mwaka 1 zaidi), Rashford anasemakana kuwa makini zaidi na kutaka kuijua ni ipi nafasi yake kwenye kikosi cha timu hiyo.

Rashford, Rashford Anajifikiria Mara Mbili Kule OT, Meridianbet
Elanga (kushoto) na Sancho (kulia)

Hatua hii inafikiwa baada ya mchezaji huyo kujikuta akisugua benchi kwa siku za hivi karibuni licha ya kuwa, alikua miongoni mwa wachezaji wenye nafasi ya moja kwa moja kwenye kikosi cha timu hiyo. Jadon Sancho na Anthony Elanga, wamekua na kiwango kizuri ambacho, kinamfanya Rashford akae benchi akiwa hana uhakika wa kucheza. Hakika, mwisho mwa msimu huu, tutajionea mengi kule Manchester United.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa