Arteta Amtaka Wenger Kurejea Arsenal.

 

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta amefichua kuwa analenga kuhakikisha kuwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Arsene Wenger, 72, anarejea klabuni kwa majukumu au wadhifa tofauti.

 

Arteta amesema kuwa ameshajadiliana na Wenger kuhusu hilo. Kocha huyo aliongoza Arsenal kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na saba ya FA kwa kipindi cha miaka 22 aliyodumu Emirates.

“Siwezi kusema chochote kwasasa, lakini ninachoweza kusema binafsi namuhitaji karibu zaidi nadhani atakuwa msaada mkubwa.

“Nadhani atakuwa msaada mkubwa kwa timu. Vitu vinachukua muda na anaweza kuwekaza katika muda huo, lakini ninachoweza kusema kwa upande wangu na kwaniaba ya kila mtu, tungefurahi angekuwa karibu zaidi.” aliongeza Arteta.

Aidha, Arteta mwenyewe alicheza miaka mitano chini ya Wenger akiwa Arsenal. Mhispania huyo alirithi mikoba ya Unai Emery mnamo Desemba 2019, miezi 19 baada ya Wenger kuondoka katika klabu ya Arsenal msimu wa 2017-2018.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.