Arteta Atoa Wito kwa Gunners Kukomesha Mfululizo wa Kupoteza Dhidi ya City

Mikel Arteta ametoa wito kwa Arsenal kubadili msururu wao wa kupoteza michezo ya ligi dhidi ya Manchester City kabla ya pambano lao huko Emirates siku ya kesho.

 

Arsenal haijapata ushindi wowote wa ligi dhidi ya washindi wa Treble tangu 2015 na kushindwa kwao hapo kesho kutaongeza mwendo wao wa kupoteza hadi mechi 13.

Arteta aliangazia kuwa timu yake imevunja misururu ya kutoshinda dhidi ya pande zingine na kuwataka wachezaji wake kufanya vivyo hivyo dhidi ya City.

Arteta alisema kuwa; “Nilipokuja hapa nadhani ilikuwa miaka 18 Old Trafford, miaka 17 nikiwa Stamford Bridge na tumefanya hivyo, kwa hivyo tubadilishe. Wasiwasi wangu pekee ni ubora wa mpinzani na hilo halina shaka na Jumapili tunapaswa kuwa katika ubora wetu kwa dakika 100. Hilo ndilo tunaloweza kudhibiti na tunahitaji kuzingatia.”

Katika michezo hii mikubwa unahitaji wachezaji wakubwa na wenye vipaji ambao wanaifanya kuhesabika. Duels ni kitu kikubwa katika mchezo ambacho kinaweza kwenda kwa njia moja au nyingine. Alisema Arteta.

Arteta alimsifu Declan Rice akisema kuwa ni mchezaji bora ambaye anaamini amezoea haraka maisha ya kaskazini mwa London baada ya kuhama kwake kutoka West Ham msimu wa joto.

Rice alihamia kwa kitita cha pauni milioni 105 mwezi Julai na ameshiriki katika mechi zote saba za ligi akiwa na The Gunners, akifunga bao la pili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester United mwezi Septemba.

Na Arteta aliangazia sifa za kiungo huyo ambazo zimemruhusu kuzoea mazingira yake mapya.

“Nikiwa na Declan, nimefurahishwa sana. Ana sifa, uwepo, uelewa wa kuwa mchezaji bora kwetu katika nafasi yake. Unapolipa kiasi hicho cha pesa unatumai kuwa watabadilika haraka sana lakini nadhani kwa ujumla amebadilika vizuri.” Alimaliza hivyo kocha huyo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.