Nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang anakiri kwamba amekuwa akihangaika sana msimu huu lakini ameamua kuufutili mbali mwenendo mbaya pindi anapokuwa mbele ya lango.
Mshambuliaji huyo wa Gabon amefunga mabao matatu tu ya ligi akiwa na Arsenal msimu huu katika mechi 15 alizocheza mpaka sasa.
Fomu mbaya ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ilichangia kuanza msimu vibaya kwa washika mtutu wa London.

“Kuanzia mwanzoni mwa msimu huu nilikuwa nikipambana sana lakini nadhani hii ni sehemu ya mpira wa miguu,” Aubameyang aliambia Sky Sports.
“Tulijitoa kwa kiasi kikubwa sana mwishoni mwa msimu hadi kushinda Kombe la FA na kufuzu kwa Ligi ya Europa kwa sababu ilikuwa muhimu sana kwa klabu.
Wakati mwingine unakuwa na heka heka na lazima upambane kadri uwezavyo. Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu na mpaka sasa haikuwa nzuri sana kutoka kwangu. Mimi bado nina maoni mazuri. Nadhani ninaweza kubadili jambo hii.” aliongeza mchezaji huyo.
MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5
Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!



Issa
Auba nyakati zimeisha
David Pere
Mshambuliaji huyo wa Gabon amefunga mabao matatu tu ya ligi akiwa na Arsenal msimu huu katika mechi 15 alizocheza mpaka sasa.
Angelina
Naona saiv hana jambo
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweli kwasababu mpambanaji sana
felister
msimu huu umekua mbaya kwake
Magdalena
Duh arsenal msimu huu wameyumba sana
Hopemwaikuka
Changamoto tu hzo
Caroline
Mpira ni kupambana
Flomena
Good news
Sania
Wajipange upya
Ernest Kimeru
Nadhani Arteta anahitaji kuangalia mfumo mzuri ambao utambeba Aubameyang
Khadija
Aangalie msimu ujao
Dorophina
Aubameyang anapotea kwenye game
Sarah
Wajipange upya
Samira
Auba ni mshambuliaji bora
Rahmal
Auba Yuko poa
warda
Bora atafute ufumbuzi