Barca Watawezana Na Haaland?

Wakati Xavi Hernandez akiendelea na juhudi za kuitengeneza Barca mpya, huko sokoni wameanza kutengeneza jina. Erling Haaland watawezana?

Haaland anaendelea kuteka vichwa vya bodi za vilabu vingi barani Ulaya. FC Barcelona, Real Madrid, Bayern Munichen, Man City, Man United na PSG zote zinatajwa kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji huyo.

Ikumbukwe, Haaland anakipengele kinachomruhusu kuondoka Borussia Dortmund kwa dau la £75M ifikapo mwezi Juni mwaka huu (2022). Hili ni dau dogo likilinganishwa na uwezo mkubwa alionao mchezaji huyo ndani ya uwanja.

Wakala wake (Mino Raiola) pia ni sababu nyingine inayochagiza usajili wa Haaland kugharimu zaidi ya dau hilo kutokana na bakshishi ambazo atahitaji kulipwa ili kufanikisha usajili wa mshambuliaji huyo.

Mino Raiola.

Inasemekana, gharama za kukamilisha usajili ni takribani £200M, hii ni pesa nyingi ambayo inaweza kuwa ni bajeti ya klabu kufanya usajili kwa madirisha mawili. Barca wataweza kulipa pesa hii wakati huu ambao, kiuchumi wana hali mbaya?

Ukiwaeka Barca pembeni, kuna Real Madrid, Man United na Man City ambao wote wanahitaji kusajili mshambuliaji. Kwa Madrid, itategemea zaidi na usajili wa Mbappe, wakifanikiwa kumsajili, huenda wakaachana na Haaland. United kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanamaliza msimu kwenye nafasi 4 za juu ili wacheze ligi ya mabingwa.

Pamoja na kuipata nafasi ya kucheza UEFA msimu ujao, bado United watahitaji kuuza wachezaji wengi (hasa wenye mishahara mikubwa) ili waweze kumsajili Haaland kwa gharama aliyonayo. City ni dhahiri, baada ya msimu huu watawekeza kwenye usajili wa mshambuliaji, lakini, ni Haaland au mchezaji mwingine?

Hakika, Julai 1, 2022 itatupa picha halisi ya hali ilivyosokoni kuelekea msimu wa 2022/23.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.