Manchester United Wafanya Mazungumzo na Richarlison

Klabu ya Manchester United imeripotiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaJI raia wa Brazil anayeychezea klabu ya Everton Richarlison kuangalia uwezekano wa kuweza kumsajiri kwenye dirisha la kiangazi.

Manchester United hivi karibuni imekuwa na mashaka na washambuliaji wake akiwemo Ronaldo na Rashford, baada ya kuwepo kwa tetesi ya kiwa mshambuliaji huyo hana furaha kwenye klabu hiyo, na endapo watashindwa kucheza michuano ya ulaya mwakani anaweza kuomba kuondoka kwenye klabu hiyo.

Manchester United

Ukiachana na Ronaldo pia Marcus Rashford ameanza kuangalia hatma yake ya baadae kwenye klabu hiyo, huku wakimtoa Martial kwa mkopo kwenda Sevilla nae hana uhakika wa kubaki kwenye kikosi pia Greenwood ameondolewa kwenye kikosi tokea apate kashfa ya kumpiga mpenzi wake.

Richarlison ambaye alijiunga na klabu ya Everton mwaka 2018 kwenye majira ya kiangazi akitokea Watford  ameicheza klabu hiyi michezo 138 na kufunga magoli 59, ingawa amekuwa hana muendelezo mzuri kwenye kiwango chake msimu hadi msimu.

Lakini Manchester United wanaona anaweza kuwa na msaada mkubwa kwenye klabu hiyo na wanataka kumuingiza kwenye mipango ya usajiri wao kwenye majira ya kiangazi.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe