Bayern Munich wapo kwenye wakati mgumu baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika mechi mbili mfululizo katika ligi kuu ya Ujerumani.
Klabu hiyo ambao ndo mabingwa watetezi nchini Ujerumani wamesuluhu leo dhidi ya Union Berlin goli moja kwa moja hivo kuwafanya vijana hao wa Julian Nagelsmann kushuka hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo nyuma ya vinara Freiburg wanaoongoza ligi kwa tofauti ya magoli baada ya kulinga alama na klabu ya Borussia Dortmund hivo Bayern wao wanakamata nafasi ya tatu.
Mwalimu Nagelsmann ana kazi ya kufanya kuirudisha timu hiyo kwenye njia ya ushindi kwani tukiachana na Bundesliga kuna michuano mingi iko mbele yao haswa michuano ya ligi ya mabingwa ulaya ambayo inaanza mapema nwezi huu huku wakiwa kundi moja na klabu ya Barcelona ambayo inaonekana kurudi kwenye ubora wao.

