Kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes na staa wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo wako vizuri wala hawana tofauti yeyote kama ambavyo ilielezwa siku ya jana.

Kuna video imesambaa kwenye mitandao ya kijamii tangu siku ya jana ikimuonesha Bruno na Ronaldo kama hawajasalimiana vizuri wakati kiungo huyo anaripoti kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ureno jijini Lisbon.bruno, Bruno, Ronaldo Hakuna Tatizo, MeridianbetKutokana na kitendo hicho kiungo wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Benfica Joao Mario leo wakati anahojiwa na waandishi wa habari ameweka wazi hakukua na tofauti yeyote baina ya wachezaji hao cha zaidi ulikua utani tu baina yao.

Joa Mario ameeleza Ronaldo alimtania mchezaji mwenzake huyo wa Manchester United baada ya kuchelewa kufika kua alikuja na boti ndo maana amechelewa ndio maneno yaliyozungumzwa kwenye video hiyo na kutafsiriwa tofauti na baadhi ya watu.bruno, Bruno, Ronaldo Hakuna Tatizo, MeridianbetKupitia ushahidi alioutoa Joao Mario inaonesha ni wazi Bruno Fernandes na Cristiano Ronaldo hawana matatizo yeyote bali ni watu walitaka kutengeneza ionekane ni ugomvi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa