Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ureno Bruno Fernandes ametimiza mchezo wa 100 kwenye ligi kuu ya Uingereza akiwa na jezi ya Manchester United leo. Kiungo huyo ametimiza michezo hiyo katika mchezo wa leo ulioikutanisha klabu yake dhidi ya Fulham United.

Kiungo fundi ambaye tangu amejiunga klabuni hapo mwezi Januari 2020 amekua mchezaji muhimu zaidi na kuhusika kwenye mabao mengi kuliko mchezaji yeyote kwa kipindi chote alichojiunga na timu hiyo.brunoBruno Fernandes amefanikiwa kushika nafasi ya nne kwenye orodha ya wachezaji waliohusika na magoli mengi kwenye timu hiyo kwenye michezo yao 100 ya kwanza ndani ya ligi kuu ya Uingereza kwenye timu hiyo akiwa nyuma ya magwiji watatu.

 

Kiungo huyo amefanikiwa kuhusika kwenye magoli 64 huku akifunga magoli 38 na kupiga pasi 26 za mabao akiwa nyuma ya Eric Cantona aliehusika kwenye mabao 84, Ruud Van Nistelrooy mabao 78 na  Dwirt Yorke mwenye mabao 66.brunoBruno Fernandes ambaye kwasasa anaonekana kuutafuta ubora wake aliokuja nao ndani ya klabu hiyo akitokea Sporting Lisbon ya Ureno bado ameendelea kua mchezaji mwenye mchango mkubwa ndani ya timu hiyo.

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa