Kiungo na nahodha msaidizi wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes amewataka wenzake kutoziangalia timu zingine ziko kwenye kipindi gani zaidi wanapaswa kujiangalia wao wenyewe kwanza.

bruno fernandesUnited ambayo imetoka kupoteza mchezo mwisho wa juma lililopita baada ya kufungwa na mahasimu wao klabu ya Manchester City kwa mabao sita kwa moja kitu ambacho kimefanya timu hiyo ni kama imerudi kwenye wakati mgumu lakini kiungo anasisitiza kutokukata tamaa na kutoangalia sana timu zingine zinafanya nini.

Man United wanaelekeza nguvu zao zote kwenye mchezo unaofuata wa ligi ya Europa siku ya alhamisi dhidi ya klabu ya Omonia Nicosia huku kiungo huyo akisema mchezo huo wanapaswa kuutazama kwa makini.

“Jukumu ni kuichezea klabu hii kubwa. Na kila mtu anapaswa kuhisi jukumu hilo, Haijalishi ni nani amevaa kitambaa uwanjani, Tunajua tuna safari ndefu lakini tunachotaka kufikia”Alisema Bruno Fernandes

bruno fernandes“Tunajua meneja anataka nini kutoka kwetu, Lakini lazima turudi kwenye matokeo mazuri na tuna nafasi ya kufanya hivyo tofauti na mchezo wa kesho” “Hatuangalii timu nyingine tunajiangalia sisi, Hili limekua tatizo kwa miaka ya nyuma kiasi cha kutaka kufanisha na timu nyingine lakini sisi hatuwezi kufanya hivo”Alisema Bruno Fernandes akifanya mahojiano na wanahabari kuelekea mchezo wao Europa League siku ya alhamisi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa