KOCHA SIMBA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Muharami Said Sultan amekamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Jeshi la Polisi Tanzania.

Taarifa hizo zimetolewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kusaya amesema kuwa Mwarami mwenye miaka 41 ni kocha kwenye timu maarufu ambayo ni Simba na aliwahi kucheza kwenye timu ya Simba zamani.

Kwa upande wa Simba wenyewe, walitola mbele na kukanusha kuwa kocha huyo hakuwa muajiriwa wa timu hiyo. Ingawa aliombwa kuwasimamia magolikipa kwa muda wa mwezi mmoja.

Na kuwaomba wanasimba wapuuze taarifa hizo kwa kuwa hazitawaathiri kwa namna yoypote ile.

Acha ujumbe