Bodi ya Shirikisho la Mpira wa miguu Barani Afrika CAF, limeidhinisha mashindano mapya ya Super League yanayotarajiwa kuhusisha timu 20 katika mkutano uliofanyika jana Cairo, Misri.
Mashindano hayo ambayo yameungwa mkono na Raisi wa CAF, Patrice Motsepe huku akisema yatafanya soka la Afrika kuwa la ushindani.
“Mashindano ya Super League Africa ni mapya kwasababu mashindano mengine yote yapo katika makubaliano na pesa inayopatikana haitoshelezi,” alisema Motsepe katika mkutano nchini Ghana mapema mwaka huu.
“Kutakuwa na mabadiliko muhimu kwa jinsi gani tunaendesha mpira wetu, ili mpira wa Bara la Afrika uweze kugundulika duniani kote. Hatutaki msaada kutoka popote. Tutafanya kazi wenyewe na nipo hapa kufanya hivyo.”
Motsepe ambaye aliingia madarakani mwezi machi, Ameihakikishia CAF ameona timu kubwa barani ulaya zikitaka kutengeneza mashindano ya Euro Super League na atajifunza kutokana na uzoefu na mapungufu hayo.
Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.


