Thomas Mueller alisema mchezaji mwenzie wa Bayern Munich Robert Lewandowski ni lazima ashinde tuzo ya Ballon d’Or siku ya jumatatu ambapo tuzo hizo zitakapo tangazwa.
Lewandowski anamatumaini makubwa ya kupata tuzo yake ya kwanza ya ballon d’Or baada ya kupata tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa FIFA mwaka 2020 kwa kuwashinda wachezaji wenye majina makubwa duniani.

“Lewy inabidi ashinde hii tuzo siku ya jumatatu, ukimwangalia kwa jinsi anavyocheza kwa sasa, hakuna mchezaji anayecheza akiwa na kiwango bora kwenye klabu wala kwenye timu ya taifa chenye muendelezo, hatuhitaji kulizungumzia hili.” alisema Mueller
Lewandowski amefunga magoli 30 msimu huu, huku Bayern Munich akifungia magoli 25, kwenye michezo 20 ya mashindano yote na magoli 5 ameifungia timu yake ya taifa ya Poland katika michezo 6.
Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.


