Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Manchester United, Carlos Tevez ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka akiwa na miaka 38 baada ya kifo cha baba yake mzazi.

Tevez amecheza katika Ligi ya kuu ya Uingereza kuanzia mwaka 2006 mpaka 2013 akivitumikia vilabu vya West Ham United, Manchester United na Manchester City.

 

carlos tevez, Carlos Tevez Astaafu Rasmi Akiwa na Miaka 38., Meridianbet

Hivi karibuni mshambuliaji huyo wa Argentina alikuwa akiichezea klabu yake ya utotoni ya Boca Junior inayoshiriki ligi kuu ya Argentina.

Tevez alimpoteza baba yake mwanzoni mwa 2021 na hiyo ni sababu kubwa iliyopelekea maamuzi ya kustaafu kucheza soka licha ya kupata ofa nyingi kutoka Ligi kuu ya Marekani MLS.

“Nimestaafu, Ninathibitisha,” alisema Carlos Tevez akihojiwa na america TV ijumaa usiku.

“Walinihaidi vitu vingi, pamoja na ofa kutoka Marekani. Lakini iko hivyo, Nilijitolea kila kitu.

“Kucheza msimu uliopita ulikua mgumu lakini niliweza kumuona mzee wangu. Nimeacha kucheza kwasababu nimepoteza shabiki wangu namba moja.” aliongeza.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa