Kulingana na Jarida la Calcio Mercato, Manchester City wamejiunga na mbio za kumsajili winga wa Juventus, Federico Chiesa.
Chelsea na Bayern Munich pia wamekuwa wakimfwatilia mchezaji huyo wa miaka 23, ambaye alikuwa na jukumu muhimu katika mbio za Italia za kutwaa taji la Euro 2020 mapema msimu huu wa joto.
Mchezaji huyo aliisaidia Azzurri kutwaa taji la Euro 2020 ambapo alifanikiwa kufunga magoli mawili katika mechi saba alizocheza katika mashindano hayo.
Chiesa amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake wa mkopo huko Juve, lakini imeripotiwa kuwa hawataki kumuuza msimu huu wa joto na wanataka kumnunua kwa mkataba wa kudumu kutoka Fiorentina.
Bado inaangaziwa kama Manchester City wataweza kumshawishi mchezaji huyo na klabu ya Juventus, baada ya dau la Chelsea la €100million (£86.3m) kukataliwa wiki iliyopita.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!


