Klabu ya Manchester City imezindua sanamu za wachezaji wao wa zamani Vincent Kompany na David Silva ambazo zipo nje ya dimba lao la Etihad kwenye jiji la Manchester.

Sanamu hizo zilizopo upande wa mashariki wa Uwanja wa City Etihad ziliundwa msanii aliyeshinda tuzo, Andy Scott na zimejengwa kwa kutumia maelfu ya vipande vya chuma vilivyounganishwa. Wakati wa usiku sanamu hizo zitaangaziwa haswa na taa za rangi ya samawati.
Vincent Kompany alisema:
“Sikutarajia kutambulika na klabu kubwa kam hii. Mke wangu ni kutoka Manchester, watoto wangu wamezaliwa Manchester, na wanarudi mahali ambapo wanaweza kuona kitu ambacho kinawakilisha kile Baba yao amefanikiwa na hicho ni kitu ambacho siwezi kuelezea.
“Mara ya kwanza niliona sanamu sikuamini jinsi ilikuwa kubwa, lakini tena, mimi nina umbo kubwa, vizuri sana! Na haswa pozi, kwangu inamaanisha mengi.”

David Silva alisema:
“Kuwepo City kulibadilisha maisha yangu. Ninajivunia kile tulichofanya pamoja na ninahisia kali kwa kutambulika hivi.
“Nilipoona sanamu hiyo mara ya kwanza, nilijisikia vizuri, nilifikiri ilikuwa kama mimi. Sanamu hii inawakilisha kweli jinsi ninavyopenda kucheza, napenda pozi ambalo mchongaji amechagua.
Inanikumbusha sana nyakati zile ambazo nilikuwa nacheza uwanjani na wakati huo ambapo nilipaswa kumtafuta mshambuliaji. ”

Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.



Sarah
Safi