Leo ni wiki ya tatu kunako Premier League ambapo kutakuwa na michezo kadhaa Chelsea, Liverpool, Arsenal na City wote watakuwa dimbani kuendeleza gurudumu la EPL. Hapa acha tuangalie mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea ambao utapigwa majira ya saa moja na nusu usiku saa za afrika mashariki.
Taarifa za Vikosi:
Mlinzi wa kushoto wa Liverpool Andy Robertson anaweza kurudi kutokana na jeraha la kifundo cha mguu kwa kuchukua nafasi ya Kostas Tsimikas.
Fabinho amerudi kwenye mazoezi kufuatia kufiwa na anaweza kurudi kwenye mchezo huu lakini James Milner hatopatikana kutokana na jeraha.
Kiungo wa kati wa Chelsea, N’Golo Kante, ambaye amekuwa akiuguza kifundo cha mguu, anaweza kuanza mchezo wake wa kwanza wa ligi msimu huu.
Cesar Azpilicueta yuko tayari kucheza mechi yake ya 300 ya Ligi Kuu.
Kurt Zouma hatakuwepo kwa sababu ya sababu za kibinafsi (hazihusiani na uwezekano wake wa kuhamia West Ham), wakati Ruben Loftus-Cheek na Christian Pulisic wanaweza kukosa kufuatia kukuwa na coronavirus hivi karibuni.
Rekodi za Kukutana:
Chelsea walishinda kwa 1-0 mara ya mwisho kukutana huko Anfiled mwezi Machi na ulikuwa ushidi wao wa saba ugenini katika EPL dhidi ya Liverpool.
The Blues wameshinda mara zote kasoro mara moja katika michezo yao 12 ya mwisho dhidi ya Majogoo katika dimba la Anfield.
Kikosi cha Liverpool Kinachoweza Kuanza: Alisson; Alexander-Arnold, Matip, Van Dijk, Robertson; Fabinho, Henderson, Thiago; Salah, Jota, Mane
Kikosi cha Chelsea kinachoweza kuanza: Mendy; Azpilicueta, Christensen, Rudiger; James, Jorginho, Kante, Alonso; Mount, Havertz; Lukaku
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.



Sarah
Chelsea ushindi