Cuisance Afeli Vipimo vya Afya Kujiunga na Leeds.


Mabingwa wa EFL waliopanda Ligi kuu EPL, Leeds United, wameshindwa kupata huduma ya kiungo wa Bayern Munich, Michael Cuisance, baada ya kufeli vipimo vya afya.

Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 21 amewahi kuchezea kikosi cha makinda wa Ufaransa. Alihamia Bayern mnamo Agosti 2019 baada ya kuagana na Borussia Monchengladbach ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).

Cuisance aliwatumikia Bayern ambao ni wafalme wa Bundesliga na Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) katika msimu wa 2019-20 na kuwafungia bao moja. Taarifa za ndani zinasema makubaliano kati ya vilabu viwili yalikuwa magumu pia.

 

Cuisance Afeli Vipimo vya Afya Kujiunga na Leeds.

Mchezaji huyo alitokea benchi katika kipindi cha pili katika ushindi wa 8-0 walioupata Bayern dhidi ya Schalke 04 katika mechi ya kwanza ya Bundesliga msimu huu.

Cuisance alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumiwa katika mchezo wa Uefa Super Cup lililowakutanisha Bayern na Sevilla mnamo Septemba 24, 2020.

Hata hivyo, aliachwa nje ya kikosi kilichotegemewa na kocha Hansi Flick katika mechi ya Bundesliga iliyoshuhudia Bayern wakichezea kichapo cha 4-1 kutoka kwa Hoffenheim mnamo Septemba 27, 2020.

 

Cuisance Afeli Vipimo vya Afya Kujiunga na Leeds.

Cuisance alisalia benchi katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) iliyoshuhudia Bayern wakizamisha chombo cha Paris Saint-Germain (PSG) kwa bao 1-0 jijini Lisbon, Ureno mnamo Agosti 23, 2020.

Leeds United ya kocha Marcelo Bielsa imesajili wachezaji wanne hadi kufikia sasa. Kikosi hicho kimewasajili Rodrigo Moreno kutoka Valencia, Diego Llorente kutoka Real Sociedad, Robin Koch kutoka Freiburg na aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Wolves, Helder Costa.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

34 Komentara

    Daah! Tumemkosa kiungo imara .

    Jibu

    Kanani tena Cuisance juu ya afya yake adi kufeli vipimo vya Afya?

    Jibu

    duh leeds wamekocha mchezaji mahili sana

    Jibu

    Afya ndo kila kitu katika maisha.

    Jibu

    Vizuri kuhijua afya yako inapendeza nafya ndio kila kitu

    Jibu

    Leeds united wamekosa bonge la kiungo

    Jibu

    Mhh kuna nn tenaaa

    Jibu

    Dah pole kwa Leeds..huyo kiungo angewafaa sana

    Jibu

    Leeds wamemkosa mchezaji mzuri sana

    Jibu

    Pole yake leeds

    Jibu

    Leeds wamekosa bonge la mchezaji

    Jibu

    Pole Sana leeds

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Wakosa mchezaji wa maana sana leeds

    Jibu

    Leeds wanatakiwa kutafuta mtu mwingine

    Jibu

    Pole

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Pole yako

    Jibu

    So sad

    Jibu

    Pole sana cuisance kwa kukosa vipimo vya afya

    Jibu

    Afya ndio mpango mzima

    Jibu

    Hii si habali njema kabisa

    Jibu

    Afya ni Bora mengne watapatikana tu

    Jibu

    Pole kijana

    Jibu

    Leeds wangepata huduma ya huyu mtu ingekua ni safi

    Jibu

    sad news

    Jibu

    Mtu makin sana leeds wamekosa mtu

    Jibu

    Duh sio poa

    Jibu

    Sio poa

    Jibu

    Dah deal limeota mbawa

    Jibu

    Daah! Tumemkosa kiungo imara .

    Jibu

    huyo kiungo angewafaa sana Leeds

    Jibu

    Ametisha sanaa

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe