Lionel Messi na Christiano Ronaldo watarudi kwenye uhasimu wao msimu huu baada ya Barcelona na Juventus kupangwa katika kundi moja katika Champions League.
Wachezaji hao wawili wametawala soka kwa zaidi ya Muongo mmoja na wanajiandaa kukutana tena baada ya timu zao kupangwa katika kundi G wakiwa pamoja na Dynamo Kiev na Ferencvaros.
Uhasimu kati ya Messi na Ronaldo ambao kwa pamoja wamefanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or mara 11 kwa kiasi kikubwa ulishika hatamu katika LaLiga, kwa ujumla wamekutana na mara 35 kwenye mashindano yote.
Takwimu zinaonesha Messi anaongoza katika makutano yao,ameshinda mara 16 na kufunga magoli 22 wakati Ronaldo ameshinda mara 10 na kufakamia nyavu mara 19.
Lakini, Ronaldo amemzidi Messi kushinda kombe la Champions League mara tano ukilinganisha na Messi aliyefanikiwa kushinda UEFA mara nne pekee na kumzidi idadi ya kufunga magoli 130 magoli 15 zaidi ya Messi.
Kuelekea katika Michezo miwili watakayo kutana acha tuangalie michezo waliyowahi kukutana hapo nyuma katika Champions League.
Barcelona 0-0 Manchester United (2007-08 Hatua ya nusu fainali)
Messi na Ronaldo ni vipaji vilivyo anza ushindani ulimwenguni wakati walipokutana kwa mara ya kwanza katika michuano ya Champions League mwezi Aprili 2008. Ronaldo alikosa nafasi ya kufunga baada ya kuchezewa rafu eneo la penati na Barca walitawala mchezo na walikuwa katika uelekeo mzuri kabla Messi nafasi yake haijachukuliwa na Bojan dakika ya 62 lakini mchezo uliisha bila kufungana.

Manchester United 1-0 Barcelona (2007-08 nusu fainali ya pili)
Messi aliendelea kuisumbua safu ya ulinzi ya Man United katika mchezo wa marudiano hatua ya nusu fainali na alikaribia kufunga baada ya kupta penati lakini mpira uliozuiliwa na kipa uliokolewa na Paul Scholes. Ronaldo alishinda taji lake la kwanza baada ya kupigiana matuta na kushinda dhidi ya Chelsea.
Barcelona 2-0 Manchester United (2008-09 fainali)
United ilikuja kuwa timu ya kwanza katika soka la kisasa kwa kutetea kucheza fainali ya Champions League kwa mara ya pili mfululizo lakini Barca walidhihirisha ubora wao katika dimba la Stadio Olimpico mjini Roma goli lililofungwa na Samuel Eto’o na kuwaweka mbele vijana wa Pep Guardiola na Messsi aliisaidia timu yake kufunga goli la pili na kufanya Barca iweke historia ya kushinda mataji matatu ndani ya msimu mmoja.
Real Madrid 0-2 Barcelona (2010-11 nusu fainali)
Messi aliiadhibu Madrid katika dimba la Santiago Bernabeu baada ya Madrid kucheza pungufu Pepe alipo kula umeme dakika ya 61 ya mchezo, Jose Mourinho aliondolewa uwanjani pia baada ya kuonesha utovu wa nidhamu. Messi alifunga goli lake ambalo bila shaka linaweza kuwa ni moja ya mbao yake bora katika soka lake, alipasiana mpira na Sergio Busquets kabla ya kuwachambua Lassana Diarra , Raul Albiol na Marcelo na kumfunga Iker Casillas na kufikisha goli la 11 katika mechi ya 11 kwenye msimu huo wa Champions League.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!


magdalena
awa vita yao haiwezi kuisha sababu kila mmoja anataka kuonesha ubabe wake kwa mwenzie
Antony Luseno
Adi leo bado haijajulikani nani bora kati ya messi na ronaldo,kila mtu ana mtazamo wake ju ya ubora wao
Adelta
Messi na Ronald bado hawajamaliza vita yao
Dorophina
Messi na Ronaldo hawawezi kumaliza bifu kwasababu viwango vyao wote vinalingana
Lydia Emmanuel Magoti
Kwanavyo waona Hawa vita vyao aviwezi kuisha kwasababu kila mtu anataka kumuonesha mwenzie ubabe
Tatu
Mafahari wawili awezi kukaa zizi koja mpaka sasahv atujajua nani mkali
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Khadija
Duh!mbona mambo
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarif meridianbet!
Elika
Hao ni mafahari tuu
Caroline
Messi na Ronaldo wanatikisa ulimwengu
Hopemwaikuka
Hv vichwa viwili ni balaaa
Rehema
Nice
aisha
Duuh kama ndiyo hivyo basi vita yao haitaweza kuisha
Mwanahamisi
Nice
Venerose
Messi na Ronaldo wote ni viungo imara
Neema
Mmh vita ya wababe
Nasra
Vita endelevu
Zuhura omary kindamba
Asante kwa taarifa
Sauda
Ligi ya mabingwa mambo ni moto.
Mwajumah
Messi na Ronaldo hawa ni mafahari wawili
Zeiyana
Messi na Ronaldo wamekua wapinzani wa mda mrefu sana bado haijajulikana nani zaidi ya mwenzie
Juliana Alex
Asante kwataharifa
Sadick
Nionavyo timu zote hazina vikosi imara sana kuleta changamoto mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya#meridianbettz
Povel
Dunia itasimama kuwa wangaliah mafahari hao watakapo menyana kwny zizi moja msimu huu kwny UEFA champions league
Saupha mohamed
Hiii haitakuja kuisha kabsaa
Shani
Hawa watu hawana wa kufanana nao wameacha historia za rekodi za kibabe
Ernest
This time itajulikana tuu who is the real GOAT
lombo
asante meridianbet kwa habar moto moto
Issa
Ni mess tu mwenye utam wake
Sabrina
Vita baridi hii
Angelina
Mafahari wawili
Amiri Kayera
Duh apo itakua noumaa
Latifa juma mohamed
Mmh ulimwengu wa soka utakuwa Moto mafahari wawili hao.
Gabriel
vikosi imara sana kuleta changamoto mashindano ya Ligi ya Mabingwa
David Pere
Adi leo bado haijajulikani nani bora kati ya messi na ronaldo,kila mtu ana mtazamo wake ju ya ubora wao
Samiah
Patachimbika