Beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ureno Diogo Dalot amefanikiwa kukamilisha dili lake la kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2028.
Klabu ya Manchester United kupitia tovuti yake na mitandao yake ya kijamii imethibitisha kua beki Diogo Dalot ataendelea kuwepo klabuni hapo kwa miaka mingine mitano, Hii imekuja baada ya mazungumzo ya muda mrefu baina ya pande hizo mbili yaani upande wa klabu na mchezaji huyo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno atasalia klabuni hapo mpaka mwaka 2028 baada ya kusaini dili hilo jipya, Lakini pia maslahi yameongezeka tofauti na yalivyokua mwanzo ikiwa ni mpango wa kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag ambaye anamuona mchezaji huyo kama mtu muhimu kwenye mipango yake ya mbeleni.
Diogo Dalot amesema amefurahia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo kubwa ulimwenguni na mipango yake ni kuhakikisha anajituma zaidi ili kuona klabu yake hiyo inapata mafanikio zaidi na zaidi siku za mbeleni ambazo yeye atakua sehemu ya klabu hiyo.
Beki Diogo Dalot alisajiliwa mwaka 2018 na kocha Jose Mourinho akiwa kijana mdogo huku akiwa hakufanikiwa kupata nafasi ya kucheza zaidi ndani ya timu hiyo, Vilevile akitolewa kwa mkopo kwenda Ac Milan mwaka 2021 lakini aliporejea alifanikiwa kuonesha ubora na kuaminiwa na kocha Erik Ten Hag na kumfanya kama sehemu ya malengo yake ya mbeleni.

