Dalot Mbioni Kusaini Mkataba Mpya

Beki wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ureno Diogo Dalot yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo ikiwa ni baada ya mazungumzo ya kina baada ya pande zote mbili.

Baada ya mazungumzo marefu yaliyochukua takribani miezi miwili hatimae taarifa zinaeleza kua beki huyo ataendelea kusalia ndani ya klabu ya Manchester United kwa muda mrefu, Diogo Dalot amekua kwenye mipango ya kocha Erik Ten Hag na ndio chachu ya kuongezewa mkataba mpya.dalotBeki huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye amekua na ubora mkubwa msimu huu na kumvutia kocha Ten Hag na kuhitaji aweze kusalia kwenye timu hiyo kwa muda mrefu,Hivo mchezaji huyo atatangazwa hivi karibuni kuongeza mkataba mpya wa kusalia ndani ya timu hiyo.

Diogo Dalot ameimarika sana msimu huu ndani ya klabu ya Manchester United baada ya kucheza kwa mkopo klabu ya Ac Milan misimu miwili iliyopita, Kutokana na ubora ambao ameuonesha msimu kocha Ten Hag amevutiwa na ubora wa beki huyo hivo akahitaji aongezewe mkataba mpya.dalotDalot alikua anafukuziwa kwa karibu na klabu ya Barcelona wakihitaji huduma ya mchezaji huyo, Lakini Manchester United wamehakikisha beki huyo anasalia kwenye viunga vya Old Trafford kwa misimu mingine kadhaa na mchezaji mwenyewe anaonesha kuhitaji kuendelea kuwepo kwenye timu hiyo.

 

Acha ujumbe