Kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen na gwiji wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Liverpool, na Bayern Munich Xabi Alonso amekua kwenye rada za mabingwa wa Ufaransa klabu ya PSG kumhitaji kama kocha mpya wa klabu hiyo.
Xabi Alonso amekua akifanya kazi iliyotukuka ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen tangu amekabidhiwa timu hiyo katikati ya msimu huu, Hivo kutokana na kiwango kikubwa ambacho amekionesha ndani ya klabu ya PSG imevutiwa na gwiji huyo na kuhitaji ainoe klabu hiyo msimu ujao.Klabu ya PSG inaripotiwa ipo kwenye mpango wa kuachana na kocha wake wasasa wa klabu hiyo Christopher Galtier mwishoni mwa msimu huu, Huku orodha ya majina ambayo yanatajwa kuwaniwa na klabu hiyo ni pamoja na gwiji huyo wa zamani wa Real Madrid ambaye anaifundisha Bayern Leverkusen kwasasa.
Xabi Alonso tangu apewe klabu ya Bayern Leverkusen amekua na uwezo mkubwa sana na kuibadilisha klabu hiyo kua yenye kutoa ushindani mkubwa kwenye ligi kuu ya Ujerumani, Huku pia akifanikiwa kuifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali ya kombe la Uefa Europa League hivo hii imefanya vilabu vikubwa kumtolea macho.Klabu ya PSG inaweza kukumbana na upinzani mkubwa kutoka katika klabu ya Real Madrid ambayo inaelezwa pia inavizia kumrudisha kocha huyo nyumbani, Hivo mabingwa hao wa Ufaransa wanaweza kukutana na upinzani huo kutoka kwa wababe hao wa soka nchini Hispania na hiyo inatokana na Alonso kufanya vizuri ndani ya Leverkusen.