Golikipa wa Manchester United David De gea ameweka rekodi ya kua mchezaji aliecheza dakika nyingi zaidi kwenye ligi kuu ya Uingereza tanga kuanzishwa kwake, Hii imekuja baada ya mchezaji huyo kucheza mchezo dhidi ya Aston Villa.

Golikipa huyo aliweza kuivuka rekodi ya aliekua pia golikipa wa Manchester United Ben Forster ambae ndio alikua mchezaji anaeongoza kwa kucheza dakika nyingi kwenye ligi kuu ya Uingereza akiwa amecheza dakika 34959, Huku De gea yeye akifikisha dakika 35039 na kuivuka rekodi ya Forster.de geaGolikipa huyo ambae amekua kwenye kiwango bora sana kwa muda mrefu klabuni hapo ndicho kitu kilichomfanya mchezaji huyo kupata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu na kufikisha dakika hizo, Kwani amekua akicheza karibuni michezo yote ya klabu hiyo.

David De gea ameshinda mataji yote na klabu hiyo kasoro taji la ligi ya mabingwa ulaya huku akivunja rekodi mbalimbali klabuni hapo kama vile kua golikipa wa kwanza klabuni hapo kua mchezaji bora wa msimu mara tatu mfululizo.de geaLicha ya kiwango hicho alichokionesha kipa huyo raia wa Hispania wamekua lakini bado kumekua na pingamizi kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana uwezo wake hafifu wa kuweza kutumia miguu yake kwa kupiga pasi sahihi na kuanzisha mashambulizi, hivo wanahitaji golikipa mwingine mwenye uwezo wa aina hiyo.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa