Golikipa wa klabu ya Manchester United David de Gea anaelezwa yupo mbioni kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa muda zaidi mazungumzo yakielezwa kufikia pazuri.
David de Gea amekua kwenye mazungumzo na klabu ya Manchester United kwa muda kidogo na taarifa zinaeleza kua mazungumzo baina ya golikipa huyo na klabu yake yapo mwishoni kabisa, Hivo ni wazi mda wowte atasaini mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Klabu ya Manchester United ilielezwa kua inatafuta golikipa mpya wa kuja kuchukua nafasi ya kipa huyo mkongwe klabuni hapo, Huku taarifa mbalimbali zikieleza kua kocha wa klabu hiyo anahitaji golikipa mwenye uwezo mzuri wa kuweza kutumia miguu yake kwenye kuanzisha mashambuliza jambo linaloonekana kama changamoto kwa De Gea.
Golikipa huyo inaelezwa yuko tayari kubakia ndani ya klabu hiyo kutokana na taarifa za ndani ya klabu hiyo, Mpaka wakati huu suala la urefu wa mkataba na mshahara vitu vyote vimeshawekwa sawa kila kitu kinatarajia kukamilika mwanzoni mwa mwezi ujao.
David De Gea ndio mchezaji anaelipwa zaidi ndani ya klabu ya Manchester United mpaka wakati huu, Lakini nyota huyo amekua kwenye ubora mkubwa ndani ya timu hiyo kwa muda mrefu kitu kinachomfanya kulipwa mshahara mkubwa zaidi na mkataba mpya ambao anatarajia kusaini maslahi yataboresha zaidi.

