Mchezaji nyota wa zamani wa Cameroon Samuel Eto’o, 40 amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon. Raisi huyo mpya ameahidi mageuzi mbalimbali kwenye michezo nchini humo.

“Lazima tuwalete wanasoka katikati ya sera zetu,” alisema baadaye. “Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba wale wanaocheza mpira huu wanapata maisha ya staha kutokana nayo.”
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Chelsea pia ameahidi kujenga angalau viwanja 10 wakati wa uongozi wake.
“Nimezungumza na jumuiya ya wafanyabiashara na tuna uhakika tutapata wawekezaji wanaofaa ambao wanaweza kuandamana nasi katika kutimiza malengo yetu,” Eto’o alisema kabla ya uchaguzi.
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa Samuel Eto’o ataendesha soka la Cameroon kwa miaka minne ijayo baada ya kuchaguliwa kuwa Raisi wa shirikisho hilo siku ya Jumamosi.
Eto’o ambaye aliwahi kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne alimshinda mpinzani wake Seidou Mbombo Njoya, makamu wa nne wa rais katika Shirikisho la Soka Afrika.
Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.


